Mkuu
wa kitengo cha Habari na Msemaji wa klabu ya Yanga, Jerry Muro
anajulikana kwa maneno mengiii utafikiri mtu wa asili ya Pwani lakini
hali halisi, Muro anatokea Kilimanjaro.
Yeye
anasema ukiwa Msemaji, basi “sema kweli”. Maneno yake yamekuwa
yakiwaudhi sana watu wa Simba lakini hivi karibuni ameonyesha hana
ugomvi na Simba baada ya kutilia suruali nyekundu ambayo ni rangi ya
Simba.
Muro
alionekana akizungumza na Msemaji wa TFF, Baraka Kizuguto huku Muro
akiwa amelamba suruali hiyo ya rangi nyekundu iliyofanya baadhi ya
mashabiki wa Simba kumshangilia wakimtania hivi: “Umependeza sana, hiyo
ndiyo rangi sahihi.”
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.