MAGURI |
Timu
ya soka ya taifa, Taifa Stars imepata sare ya bao 1-1 katika mechi ya
kirafiki dhidi ya Kenya ‘Harambee Stars’ katika mechi ya kirafiki
iliyochezwa kwenye Uwanja wa Moi Kasarani jijini Nairobi.
Elius Maguri alikuwa wa kwanza kuifungia Taifa Stars bao katika dakika ya 33 akiunganisha krosi safi ya Juma Abdul.
Lakini
dakika sita baadaye, Kenya wakasawazisha kupitia nahodha wao Victor
Wanyama anayekipiga Southampton ya England ambaye alifunga kwa mkwaju wa
penalti iliyolalamikwa kuwa siyo.
Pamoja na mabao hayo, Stars ilionekana kutawala zaidi kipindi cha pili mwisho na hata baada ya kuanza kipindi cha pili.
Hata hivyo, tatizo lilionekana ni kutokuwa na mipango imara katika safu ya ushambulizi.
Mechi hiyo ya Stars ni maandalizi ya kuivaa Misri mechi itakayochezwa Juni 4 jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.