Moyo unatumika kuficha siri nzito ambazo kwa macho hatuzioni. Wakati mwingine ni mbaya mno hadi inafikia hatua ya wengine kupata mshtuko wa moyo kwa kushindwa kuvumilia maumivu au furaha walizonazo. Adui wa moyo ni moyo na furaha ya moyo ni moyo
.
Unadhani tabasamu linalotoka kwenye paji la uso la Juan Mata ni la furaha? La hasha moyo wake umejeruhiwa mno lakini kuficha kidonda chake ametumia tabasamu pana kufunika maumivu anayoyapata. Hii si kwa Mata pekee vipi kwa Yaya Toure? Moyo wake hauna raha tangu uliposikia jina la Pep Guardiola litaingia kwenye kambi ya Etihad. Ndivyo maisha yalivyo ufundi wote alionao Mata hauna kitu kwa Mourinho vivyohivyo kwa Toure
.
Kabla ya Mourinho kurudi kwa mara ya pili kwenye timu ya Chelsea Juan Mata ndiyo alikuwa kila kitu pale darajani. Mikel Obi alipokuwa anafanya shughuli chafu za kukaba aliuchukua mpira na kumpa fundi Mata ili aupleke sehemu sahihi ambayo yeye anajua.
Mata alivutia kila alipokuwa na mpira. Alivutia kwa kila dribble a
liyoifanya na alivutia kwa kila pasi aliyopiga. Mwisho wa yote mashabiki wa Chelsea walimuingiza kwenye mioyo yao na kumpenda mno.
Kwa kipindi kile hata kama haukua shabiki wa Chelsea lakini ilikuwa lazima ufurahi kumuona Mata akiwa kwenye uzi wa bluu akiutumikisha mpira alivyotaka. Pamoja na mioyo ya mashabiki wa United kuvuja damu lakini hakuna aliyemchukia Mata kwa ile pasi murua ya kuchop kwa Demba Ba.
Mata alipata mateso mno baada ya kurudi Mourinho ambaye hakuvutiwa naye ilhali Mata alikuwa mchezaji bora wa mwaka wa Chelsea kwa miaka miwili mfululizo. Mourinho hapendi mfalme mwingine sehemu anayokuwa yeye. Yeye ndiye mfalme. Yeye ndiye anataka jina lake liimbwe zaidi na zaidi.
Ufalme wa Mata ulipotea kama mshumaa na alimuuza Manchester United ambako sasa Mourinho ndiyo anaenda kufanya kazi. Mpiga gitaa huyu wa Hispania sidhani kama moyo wake unafuraha. “Nipo tayari kugombania namba” hicho ndicho alichosema Mata baada ya Jose Mourinho kutangazwa kuwa kocha wa United.
Kwa upande wa Yaya Toure ilikuwa ni lazima aondoke Barcelona ili damu ya nyumbani ipate nafasi. Wacatalunia wanapendana sana. Wakati Toure anapiga kazi ngumu pale kwenye dimba la Camp Nou alirahisisha kila kitu kwa watu wa mbele walioongozwa na Ronaldinho,Eto’o na Iniesta.
Lakini Toure hakuingia kwenye moyo wa Guardiola kwa mtindo wake wa uchezaji. Pep ni muumini wa style ya Tik-Tak ambayo ndiyo uti wa mgongo wa Barcelona kwa kupiga pasi nyingi kwenye nafasi. Nipe nikupe, nakupa unanipa tena kisha nakupa tena ilikuwa burudani mno.
Yaya Toure aliuzwa Manchester City ambako Guardiola anaingia kufanya kazi. Toure ni mfalme pale Etihad ukimwacha Aguero lakini moyo wake umepata majeraha makubwa yanayopunguza furaha yake kwa Guardiola kuingia alipo yeye. Maisha yataendelea kuwa magumu sababu Pep mtindo wake ni ule ule wa Tik Tak popote anapoenda. Toure hana maisha tena pale Etihad lazima ataondoka kutafuta malisho mapya
.
Wakati unajiuliza kuhusu Mata kwa Mourinho. Ulishajiuliza ili swali la Mourinho kwa nini anampenda sana Mesut Özil!? Jose kashindwa kuficha mahaba yake kwa Mjerumani huyo fundi wa kupiga pasi za mwisho hasa pale alipochukua jezi yake baada ya mpira kuisha kati ya Arsenal na Chelsea.
Jiulize tena Mata na Özil wanatofauti sana katika ufanyaji wa kazi zao? Labda moyo wa Mourinho unaweza kujirudi kama atamfanya Mata kuwa Özil wake wa Old Trafford kwa kumtengenezea watu wanaomzunguka yeye kama alivyofanya wakati yupo na Özil kule Hispania kwenye timu ya Real Madrid.
Katika kazi ya Mourinho, Mata anaweza kufikiriwa tena na tena lakini katika kazi ya Guardiola sioni Toure akiendelea kuishi pale Etihad mwisho wake umefika
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.