Klabu
ya Genk ya Ubelgiji imesema itamwachia Mbwana Samatta Juni Mosi ili kuja
nchini kujiunga na Taifa Stars lakini si kwa ajili ya mechi ya kirafiki
dhidi ya Kenya.
Hali kadhalika, TP Mazembe nayo imekataa kumuachia Thomas Ulimwengu kwa ajili ya mechi hiyo kwa kuwa ina majukumu muhimu.
Msemaji wa TFF, Alfred Lucas amethibitisha hilo kuwa TP Mazembe itaivaa AS Vita katika mechi yenye upinzani mkubwa.
“Kweli
hilo limethibitishwa na Mazembe kuwa wana majukumu muhimu ikiwemo mechi
hiyo dhidi ya AS Vita ambayo kwao ni mechi ya upinzani mkubwa,” alisema
Alfred.
Stars
iko nchini Kenya kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya wenyeji wake
Harambee Stars ikiwa ni maandalizi ya kuivaa Misri jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.