KOCHA
Zinedine Zidane amesema nyota wake, Cristiano Ronaldo yuko fiti kwa
asilimia 100 kwa ajili ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini
amekiri Mreno huyo atalazimika kucheza na maumivu ili kumaliza mechi
hiyo.
Mfaransa
huy na mchezaji wa zamani wa Real Madrid amesema hakuna wasiwasi
Ronaldo ataanza dhidi ya mahasimu wao, Atletico Madrid na anatarajia
atamalaiza mechi.
Ronaldo aliumia Jumanne baada ya kugongana na Kiko Casilla kwenye mazoezi na akalazimika kutoka nje kutubiwa na nesi mguu wake.
Zidane
alisema maneno kama hayo kabla ya mchezo wa Nusu Fainali ya michuano
hiyo dhidi ya Manchester City Uwanja wa Etihad mwezi April, baada ya
Ronaldo kuumia nyama. Lakini Mfaransa huyo alisistiza jana:
"Si
kitu kile kile. Alikuwa anasikia maumivu makali, lakini kwa sasa yupo
fiti kwa asilimia 100, na zaidi ya hayo anacheza fainali.
"Unapocheza
fainali kama unasikia maumivu yoyote, unajipa ujasiri wa kuahau.
Alikuwa anasikia maumivu kidogo, lakini si kitu na kesho (leo) atakuwa
fiti kwa asilimia 100," amesema.
Sergio
Ramos, aliyefunga bao la kusawazisha dakika ya tatu ya muda wa nyongeza
katika fainali ya mwisho timu hizo kukutana miaka miwili iliyopita
ikishinda kwenye muda wa nyongeza, amesema atajituma kurudia matokeo
hayo.
Ramos,
ambaye pamoja na wachezaji wenzake, alipigwa picha akiwa na nyota wa
Hollywood, Richard Gere na mpenzi wake, Alejandra Silva, na akasema:
"Tumepambana mno ili kufika fainali na tuko hatua moja kufika kileleni.
Tunakwenea kuacha ngozi zetu uwanjani ili kupata taji,".
Wasanii
wa Italia, Andrea Bocelli na nyota wa muziki Alicia Keys watatumbuiza
kabla ya fainali hiyo Uwanja wa San Sito mjini Milan, Italia usiku wa
leo.
Mwigizaji
Gere mwenye umri wa miaka 66, na Silva mwenye umri wa miaka 33
walikuwepo kwenye mazoezi ya Real jana na leo watawasapoti vigogo hao wa
Hispania.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.