KLABU
ya Barcelona imethibitisha Dani Alves ataondoka, lakini imekana kuwa na
mpango wa kumchukua Hector Bellerin wa Arsenal akazibe pengo lake.
Alves amekuwa kazini Nou Camp tangu asalijiwe kutoka Sevilla miaka nane iliyopita.
Mkurugenzi
wa Usajili, Roberto Fernandez amesema: "Dani ameamua kuondoka na
tunapaswa kukubali uamuzi wake. Ameithibitishia klabu anachotaka ni
kuondoka.
"Tunapaswa
kukumbuka kwamba amemaliza Mkataba wake mwaka uliopita, lakini
hatukuweza kusajili mchezaji yeyote kwa sababu ya adhabu ya kufungiwa
kusajili na FIFA na hivyo yalikuwa mazingira magumu kwetu na akaongeza
Mkataba.
Lakini sasa anatafuta mazingira mazuri zaidi kwake,".
Alves amekaribia kumalizana na Juventus na wakala wake, Dinorah Santana pia anafanya mazungumzo na Paris Saint-Germain.
Beki
huyo wa kulia anaweza kupewa dau zuri kwa sababu katika Mkataba wake
mpya, kwa sababu wakati anaongeza Mkataba Barca mwaka jana,
walikubaliana vigogo hao wa Hispania hawatapa ada ya uhamisho akiondoka
Camp Npu.
Mkongwe huyo wa Brazil mwenye umri wa miaka 33, anaondoka Barca baada ya miaka nane, akishinda mataji 23.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.