Kweli
Simba wameamua, tayari beki Janvier Besala Bokungu raia wa DRC, ametua
Dar es Salaam kimyakimya ili kumalizana na uongozi wa Msimbazi.
Bokungu
ni beki wa zamani wa TP Mazembe, kama unakumbuka vizuri ndiye
walimchezesha katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba ikakata
rufaa kwenye Shirikisho la Soka Afrika (Caf), TP Mazembe wakaondolewa
mashindanoni na Simba kupata nafasi ya kucheza na Wydad Casablanca ya
Morocco.
“Tayari
wametua hapa nchini na wataanza mazungumzo na taratibu nyingine, maana
Bokungu alikuwa Esperance ya Tunisia. Mimi ninaamini atasajiliwa Simba
maana kiwango chake kipo juu tu,” kilieleza chanzo.
Caf,
ilitangaza uamuzi wa kuiondoa TP Mazembe Mei 14, 2011 na mechi
ikachezwa kwenye uwanja huru wa Petrojet jijini Cairo, Misri, Simba
ikatandikwa mabao 3-0, hiyo ilikuwa Mesi 28, 2011.
Bokungu
yuko jijini Dar es Salaam pamoja na kiungo mwingine raia wa DR Congo
pia wakisubiri ‘kuonwa’ na makocha au watu maalum kabla ya kusaini
mkataba kama Simba wataridhika nao.
Habari
za uhakika kutoka ndani ya Simba zinasema, pamoja na Bokungu na kiungo
huyo, mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Blagnon Frederick kutoka Africa
Sports ya Ivory Coast alitarajiwa kuwasili jana.
“Kama
si jana, basi atatua kesho (leo) tayari kabisa kuanza majaribio na
kufanyiwa vipimo kama atakuwa amefuzu,” kilieleza chanzo. Kwa kipindi
hiki Blagnon ndiye mfungaji anayeongoza kwa kupachika mabao katika ligi
hiyo kwao Didier Drogba.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.