Mmoja wa Wakurugenzi wa kampuni ya
Bin Slum Tyres, Mohammed Bin Slum (katikati) akisaini mkataba pamoja na
Katibu Mkuu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe (kushoto) na Meya wa jiji la
Mbeya, David Polela.
|
Kampuni
ya Binslum Tyre kupitia betri zake imara za magari za RB, leo Alhamisi
imeongeza mkataba wa kuendelea kuidhamini timu ya Mbeya City kwa miaka
mingine miwili mingine baada ya ule wa awali kumalizika.
Binslum
kwa mara ya kwanza kupitia RB ambazo ni kwa ajili ya magari makubwa na
madogo, iliingia mkataba na timu hiyo Juni, 2014 ambapo umemalizika
mwezi huu, huku huu wa sasa ambao una thamani ya shilingi milioni 300,
ukitarajiwa kumalizika Juni, 2018.
Katika
hafla fupi ya kusaini mkataba huo iliyofanyika kwenye ofisi ndogo za
kampuni hiyo zilizopo Kariakoo jijini Dar, mbali na waandishi wa habari,
pia ilihudhuriwa na Mtendaji Mkuu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe,
Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, David Polela Mwashilindi na Makamu
Mwenyekiti wa Binslum, Mohammed Binslum.
Binslum
amesema: “Tumeona tuna kila sababu za kuendelea kuidhamini tena Mbeya
City kwa miaka mingine miwili baada ya kuonekana ni mabalozi wazuri wa
bidhaa zetu.
“Kwenye
mkataba wa awali walifuata kile ambacho tulitaka wakifanye, hivyo
hatukuwa na maswali mengi ya kujiuliza kabla ya kuongeza mkataba.
Mkataba huu mpya una thamani ya shilingi milioni 300.”
Naye
Kimbe alisema wataendelea kuwa mabalozi wazuri wa kampuni hiyo katika
kuzitangaza bishaa zao na wanaishukuru kwa ushirikiano wao kwa kipindi
chote cha mkataba wa awali na wanaamini itakuwa hivyo kwa mkataba huu
mpya.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.