Rais wa Argentina Mauricio Macri
amemwita nyota wa soka wa nchi hiyo Lionel Messi kwa lengo la kumuomba
atengue maamuzi yake ya kujiuzulu kucheza soka la kimataifa.
Messi
alifikia maamuzi hayo baada ya timu yake kushindwa kwa mara ya pili
mfululizo katika fainali za Copa America huku akiwa miongoni mwa
wachezaji waliokosa mikwaju ya Penalti. ''Amemwita na kumueleza namna
anavyoona fahari kwa kiwango kizuri kilichoonyeshwa na timu yake katika
michuano hiyo huku akimtaka asisikilize maneno ya watu'' ilisema msemaji
wa Rais Macri.
Ndani ya miaka mitatu Messi ametinga katika fainali tatu
tofauti moja ikiwa ni ya kombe la dunia nchini Brazili mwaka 2014
ambapo walipoteza dhidi ya Ujerumani,na nyingine mbili za Copa America
moja ikiwa mwaka 2015 na 2016 zote timu yake ikipoteza dhidi ya Chile.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.