Ndugu wawili England na Wales leo wanakutana katika muendelezo wa michuano ya Euro, mchezo wa kundi B utakaofanyika kunako dimba la Stade Felix Bollaert-Delelis lililopo manispaa ya Lens.
Wales wanaingia katika mchezo huu wakiwa kileleni mwa kundi baada ya kushinda mchezo wa awali kwa magoli 2-1 dhidi ya Slovakia, huku nyota wa timu hiyo Gareth Bale akirusha kijembe kwa England kwa kusema kwamba hakuna mchezaji wa timu hiyo angeweza kupata nafasi katika kikosi cha Wales.
Bales anaongeza kwa kusema kuwa wachezaji wa Wales wana moyo wa kujitolea zaidi kwa taifa lao kuliko wapinzani wao, kitu ambacho kocha wa England Roy Hodgson amekiita ni ‘kuwakosea heshima’.
Kiungo wa Arsenal Aaron Ramsey, vile vile amekazia kauli ya Bale kwa kudai kwamba timu yao ni nzuri na anamini ari waliyonayo ni sababu tosha ya kuibuka na ushindi dhidi ya wapinzani wao katika mchezo wa leo.
“Tumepambana sana kufika hapa. Sasa tunakula matunda yetu,” amesema Ramsey.
Tumekuwa pamoja wakati wa taabu na raha. Kila mmoja anapigania timu kuhakikisha tunafanikiwa.”
Kwa upande wake, Winga wa England Adam Lallana, ambaye alicheza katika mchezo wa kwanza dhidi ya Russia ulioisha kwa sare ya bao 1-1 jijini Marseille, amewaasa wachezaji wenzake kutoyumbishwa na Bale na badala yake jicho lao watupie kwenye mchezo wenye huku akiwatahadharisha pia kumchunga Ramsey na mchezaji mwenza wa Liverpool Joe Allen.
“Ninafurahi sana kucheza na Joe Allen na najua namna gani ana kipaji kikubwa. Aaron Ramsey ni mtu mwingine mwenye kipaji cha aina yake, hivyo tusipoteze muda kumchunga Bale pekee na kusahau wachezaji wengine hatari,” Lallana amesema
“Kitu cha msingi ni kuheshimu timu yote kwa ujumla na kuangalia ubora wa udhaifu wao ili kujua namna gani ya kupambana nao.”
Mapambano ya uso kwa uso kati ya timu hizi mbili (Hea-to-head).
- Hii inakuwa ni mara ya 102 kwa England na Wales kupambana, licha ya kwamba ni mara ya kwanza kwao kukutana katika mashindano makubwa ulimwnguni. wameshinda mara 66, Wales mara 14 na wametoka sare mara 21.
- Wales hawajaifunga England tangu mara ya mwisho walipopata ushindi wa bao 1-0 mwaka 1984, goli lililofungwa na Mark Hughes wakati huo akiwa ndio anacheza kwa mara ya kwanza kwenye timu ya taifa.
- England wameshinda michezo yao yote minne iliyopita dhidi ya Wales bila ya kuruhusu goli. Wlishinda 2-0 nyumbani na 1-0 ugenini wakati wa kufuzu fainali za Kombe la Dunia mwaka 2006, vile vile wakashinda 2-0 ugenini na 1-0 nyumbani wakati wa michezo ya kufuzu fainali za Euro mwaka 2012. Ashley Young ndiyo alifunga goli la mwisho.
- Kocha wa Wales Chris Coleman alishawahi kufundishwa na kocha wa England Roy Hodgson. Alicheza mchezo mmoja tu akiwa Blackburn Rovers mwaka 1997-98
- Coleman na Hodgson wote wamewahi kufundisha timu ya Fulham na kucheza pia kwenye timu ya Crystal Palace.
- England wamefuzu michuano ya Euro mwaka huu bila ya kupoteza mchezo wowote wakiungana na timu za Ufaransa (1992, 2004), Jamhuri ya Czech (2000) na Ujerumani na Uhispania (wote mwaka 2012)
- Hii ni mara ya pili kwa England kupambana na timu kutoka UK katika michuano ya Ulaya, mara ya mwisho walicheza dhidi ya Scotland mwaka 1996 na kushinda magoli 2-0.
- England walipiga mashuti 8 kwenye mchezo uliopita dhidi ya Russia katika kipindi cha kwanza, ikiwa ni mashuti mengi zaid tangu walivyofanya hivyo mara ya mwisho dhidi ya Croatia mwaka 2004 walipopiga mashuti 11.
- England wameshindwa kufunga zaidi ya goli moja katika michezo yao 13 kati ya 14 waliyocheza katika ushiriki wao kwenye mashindano makubwa ulimwenguni.
- Kwa kufunga goli dhidi ya Russia, Eric Dier anakuwa mchezaji wa nane wa Tottenham kuifungia England goli katika michuano mikubwa.
- Wales wameruhusu goli katika kila mchezo kati ya michezo yao mitano ya mwisho (ikiwemo ya kirafiki), hiyo ikiwa ni takwimu mbaya zaidi kwao tangu March 2013 (mara 11).
- Aaron Ramsey amehusika kweye magoli matatu kwenye michezo mitatu ya mwisho ya Wales (kafunga magoli 2 na kutoka pasi moja ya goli).
- Bale ni mchezaji wa kwanza wa UK kufunga goli lililotokana na mpira wa adhabu katika michuano ya Euro mwaka huu.
- Wales ndio timu ya kwanza ya Kiingereza kushinda mchezo wa ufunguzi katika michuano ya Euro mwaka huu.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.