FAHAMU WACHEZA SOKA 10 AMBAO NI MAPACHA WA KUFANANA SAANA


Pacha 3




Mchezo wa soka ni kama familia moja lakini inapendeza sana kuona pale ndugu wa damu wanapocheza kwenye timu moja au wakati mwingine kukutana kila mmoja akiwa kwenye timu tofauti. Leo tunakuletea wacheza soka maarufu ambao ni ndugu wa damu, lakini kama haitoshi wachezaji hao ni mapacha wa kufanana.

Inawezekana ukawa huwafahamu baadhi yao laikini hii ndiyo fursa yaw ewe kuwafamu, na inawezekana pia ukawa unamfahamu mmoja lakini kumbe ana ndugu yake ambaye hukuwa unamfahamu kabla.

Ungana nami hapa nikupe list ya wachezaji ambao ni mapacha wa kufanana…

10. Rafael na Fabio da Silva

Pacha

Kwa pamoja wamezaliwa July 9, 1990. Pacha ya da Silva walianza soka lao kwenye klabu ya Fluminense ya Brazil kabla ya kujiunga na Manchester United mwaka 2008. Hawakuwa na mafanikio makubwa kwenye timu yao ya taifa, Rafael na Fabio wamecheza mechi mbili tu za kimataifa.

afael kwa sasa anacheza Olympique Lyonnais ya Ufaransa inayoshiriki Ligue 1 wakati Fabio yeye anacheza England kwenye klabu ya Cardiff City inayoshiriki Championship.
  1. Lars na Sven Bender
Pacha 1

Wachezaji hawa wa kimataifa wa Ujerumani Lars na Sven Bender walizaliwa April 1989 wakati huo West Germany wakati huo Ujerumani ikiwa imegawanyika katika pande mbili, Mashariki na Magharibi. Lars anacheza kama kiungo kwenye klabu ya Bayer Leverkusen whiles wakati Sven akicheza kama kiungo mkabaji kwenye klabu ya Borussia Dortmund, wote kwa pamoja hawana mafaniko kwenye timu ya taifa wakiwa wamekosa michuano ya kombe la dunia la mwaka 2014.

8. Hamit na Halil Altintop

Pacha 10

Mapacha hwa wa kufanana walizaliwa December 8, 1982 Gelsenkirchen, Germany. Hamit ni kuiungo anacheza nafasi tofauti, anaweza kucheza kama kiungo wa ulinzi, kiungo mshambuliaji na wakati mwingine anacheza kwenye wing zote mbili. Anafahamika zaidi kwa kupiga mipira mirefu.

Hamit alishinda tuzo ya goli bora la mwaka 2010 (2010 Puskas award) wakati ndugu yake Halil anacheza kwenye klabu ya Augsburg ambaye anaweza kucheza kama mshambuliaji wa kati au winger na wakati mwingine kiungo mshambuliaji.

7. Ramiro na Rogerio Funes Mori

Pacha 3

Baada ya kusajiliwa kutoka River Plate kwenda Everton, Ramiro amekuwa kwenye kiwango bora na sasa amekuwa kwenye radar za miamba ya soka la Spain FC Barcelona , anapacha mwenzake wa kufanana Rogerio na walizaliwa March 5, 1991 Mendoza, Argentina.

Baada ya familia yao kuhamia USA mwaka 2001, Ramiro alijiunga natimu ya vijana ya FC Dallas lakini baada ya muda alirejea Argentina na wote kwa pamoja na pacha wake Rogerio walisajiliwa na klabu ya River Plate. Rogerio kwa sasa anacheza soka lake nchini Mexico kama mshambuliaji wakati Ramiro yeye yupo Everton ya England.

Ramiro Funes Mori kwasa anaiwakilisha Argentina kwenye michua Copa America Centenario inayoendelea huko Marekani.

6. Jose na Juanmi Callejon

Pacha 4
Juan Miguel”Juanmi” Callejon Bueno na Jose Callejonwalizaliwa kwenye kitongoji cha Motril, Granada, Spain February 11, 1987 na wote kwa pamoja wali-graduate kwenye klabu ya Real Madrid.
Juanmi anacheza ligi ya Bolivia kwenye klabu ya Club Bolivar wakati Jose yeye anakipiga Napoli ya Italy.

Jose Callejon alicheza mchezo wake wa kwanza kwenye timu ya taifa ya Hispania mwaka 2014 na tangu wakati huo amechea mara mbili tu huku ndugu yake Juanm akiwa bado hajacheza hata mchezo mmoja kwenye timu ya taifa.

5. Aleksei na Vasili Berezutski

Pacha 5

Mapacha hawa wa kufanana walizaliwa June 20, 1982 Moscow, Russia. Wanacheza katika nafasi ya ulinzi kwenye klabu ya CSKA Moscow. Vasili anaweza kucheza kama kiungo au wing full-back, alifunga bao la kusawazisha dhidi ya England dakika ya 90+3 kwenye sare ya bao 1-1 kwenye michuano ya Euro 2016 katika hatua ya makundi kabla ya timu yake kukutupwa nje ya mashindano.
Aleksei anasifika kwa kuwa beki anaeshambulia zaidi. Wote kwa pamoja wana umri wa miaka 34.

4. Philipp na David Degen

Pacha 6

Philipp na David Degen walizaliwa February 15, 1983 Liestal,Switzerland. Hawa wana mchanganyiko wa Uholanzi kwa upande wa mama yao.

David amestaafu na alikuwa anafahamika kwa kutokana na kuichezea klabu ya Young Boys ya Switzerland kati ya mwaka 2008 hadi 2012 huku ndugu yake Philipp akiwa bado na mkataba na klabu ya FC Basel.

Mapacha hawa waliteuliwa kuichezea timu ya taifa ya Switzerland kwenye michuano ya kombe la dunia iliyofanyika Ujerumani mwaka 2006.

3. Martin na Marcus Olsson

Pacha 7

Marcus Jonas Munuhe Olsson na Martin Tony Waikwa Olsson jamaa hawa ni wasweden waliozaliwa May 17, 1988. Marcus anacheza kama mlinzi wa pembeni wa klabu ya Norwich City inayoshiriki ligi daraja la kwanza (Championship) nchini England  wakati Martin anakipiga kama kiungo au beki wa pembeni kwenye klabu ya Derby County inayoshiriki Championship pia.

Martin alikuwepo kwenye kikosi cha Sweden kilichoondolewa kwenye michuano ya Euro 2016 inayoendelea nchini Ufaransa. Wote wanaasili ya Kenya pia, mama yao ni mkenya lakini baba yao ni mswedish.

2. Florentin na Mathias Pogba

Pacha 8

Florentin na Mathias Pogba hawa ni wachezaji wa kimataifa wa Guinea waliozaliwa August 1990 Conakry, Guinea. Ni wakubwa kuliko kiungo wa kimataifa wa Ufaransa Paul Pogba.
Mathias kwa sasa anacheza kwenye ligi ya Scotland akiwa na timu ya Partick Thistle kama mshambualiaji wa kati na tayari ameichezea mara mbili timu ya taifa ya Guinea tangu mwaka 2013 wakati pacha mwenzake Florentin anacheza kama beki kwenye klabu ya Saint-Etienne ya France.

1. Josh na Jacob Murphy

Pacha 9

Wachezaji wa England Josh na Jacob Murphy walizaliwa February 24, 1995.
Kwa pamoja wanaitumikia klabu ya Norwich lakini wote wametolewa kwa mkopo, Jacob amepelekwa Coventry City wakati Josh yeye yupo Milton Keynes Dons. Wote kwa pamoja wameitumikia timu ya taifa ya vijana ya England na wanaundugu na Tommy Parkin mchezaji wa zamani wa Ipswich Town.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.