IBRA ‘AZUIWA’ KUONDOKA KAMBINI SWEDEN KWENDA KUSAINI MAN UNITED!












    KUKAMILISHA kwa dili ya Zlatan Ibrahimovic kujiunga na Manchester United kumekwamishwa kutokana na amri ya Kocha wa Timu ya Taifa ya Sweden, Erik Hamren, kumzuia kuondoka Kambini kwenda Jijini Manchester.

    Ibrahimovic yupo na Kikosi cha Sweden huko France ambacho kitashiriki Fainali za EURO 2016 na wapo Kundi E pamoja na Belgium, Republic of Ireland na Italyna Jumatatu watacheza Mechi yao ya kwanza na Republic of Ireland huko Stade de France, Paris.

    Ibrahimovic, mwenye Miaka 34, anaihama Paris Saint-Germain baada ya kumaliza Mkataba wake na kuwa Mchezaji Huru.

    Inaaminika Ibrahomivic tayari ameshaafikiana na Man United kuhusu maslahi yake binafsi.
    Kocha wa Sweden, Hamren, akinukuliwa na Gazeti la Sweden Goteborgs-Posten, amesema; “Wachezaji wana ofu wakati wa michuano hii na hilo siwezi kuzuia lakini si sahihi kwa Zlatan kuruka kwenda Manchester.” 
      
    Pia Hamren alisisitiza kuwa hana wasiwasi kwamba habari hizo zitamuathiri Staa huyo au Kikosi chake pale alipoeleza: “Nina hakika asilimia 100 haitamuathiri Zlatan, yupo kwenye biashara hii kwa muda mrefu!” 

    Endapo Ibrahimovic atakamilisha dili ya kuhamia Man United basi atakuwa Mchezaji wa Pili baada ya Beki kutoka Ivory Coast, Eric Bertrand Bailly, alietoka Villareal ya Spain kuhamia Man United chini ya Meneja Mpya Jose Mourinho.

    KIFUATACHO NI KIOSI CHA MAN UNITED KILICHOWASILISHWA RASMI KWA LIGI KUU ENGLAND HAPO MEI 21:

    MAKIPA: Joel Castro Pereira, David De Gea, Dean Henderson, Sam Johnstone, Kieran O'Hara*, Sergio Romero.

    MABEKI: Tyler Blackett, Daley Blind, Cameron Borthwick-Jackson, Matteo Darmian, Sadiq El Fitouri*, Tim Fosu-Mensah, Phil Jones, Donald Love, Paddy McNair, Matthew Olosunde, Regan Poole, Tyler Reid, Joe Riley*, Marcos Rojo, Luke Shaw, Chris Smalling, Axel Tuanzebe, Antonio Valencia, Guillermo Varela, Tyrell Warren, Ro-Shaun Williams.

    VIUNGO: DJ Buffonge, Michael Carrick*, Marouane Fellaini, Sean Goss, Callum Gribbin, Ethan Hamilton, Josh Harrop, Ander Herrera, Jesse Lingard, Scott McTominay*, Juan Mata, Andreas Pereira, Devonte Redmond*, Joe Rothwell*, Morgan Schneiderlin, Bastian Schweinsteiger, James Weir*, Matty Willock.

    MAFOWADI: Zak Dearnley, Memphis Depay, Josh Doughty*, Ashley Fletcher*, Adnan Januzaj, Will Keane, Anthony Martial, Demi Mitchell*, Marcus Rashford, Wayne Rooney, James Wilson, Ashley Young.

    *Mchezaji aliepewa Ofay a Mkataba.
    **Jina la Eric Bailly lilikuwa bado halijapelekwa.
    Share on Google Plus

    About Unknown

    This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
      Blogger Comment

    0 comments:

    Post a Comment

    Note: Only a member of this blog may post a comment.