Hii ni siku mbaya kwa soka la Argentina, baada ya kushindwa kutwaa taji la Copa America kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Chile, wachezaji wa Argentina mmoja baada ya mwingine wamekuwa wakitangaza kustaafu kuichezea timu yao ya taifa.
Mchezaji wa kwanza kutangaza kustaafu kuitumikia timu hiyo alikuwa Leo Messi ambaye alitangaza uamuzi huo muda mfupi baada ya mchezo dhidi ya Chile kumalizika.
Muda mfupi baadaye striker wa Manchester City Sergio Aguero na mlinzi wa kati wa FC Barcelona Javier Mascherano nao pia walitanga kuachana na timu soka la kimataifa.
Kama vile haitoshi, ripoti kutoka Amerika ya Kusini zinadai kuwa, Angel Di Maria, Ezequiel Lavezzi, Gonzalo Higuain na Lucas Biglia nao pia wameamua kutundika daruga kuitumikia Argentina.
Laikini kocha wa timu hiyo Tata Martino hajachukua uamuazi wa kuikacha timu hiyo.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.