Wakati
TP Mazembe inajiandaa kuja jijini Dar es Salaam kucheza na Yanga,
mmiliki wake Moise Katumbi Chapwe amehukumiwa kwenda jela.
Chapwe ,51, aliyeondoka nchini DR Congo mwezi Mei, mwaka huu kwenda Ulaya, amehukumiwa kwenda jela miezi 36.
Katumbi
ambaye yuko nje ya DR Congo, amepatikana na hatia ya kuuza moja ya mali
zake katika eneo la Lubumbashi ikionekana hakufuata sheria za nchi hiyo
huku akijua ni makosa.
Hata
hivyo, tajiri huyo ambaye alihukumiwa bila kuwepo mahakamani,
inaonekana ameingia kwenye tatizo hilo baada ya uamuzi wake wa kuamua
kugombea urais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya DR Congo.
Uamuzi
huo unaonekana kumkera Rais Joseph Kabila aliye madarakani tokea mwaka
2001 ameamua kuendelea kugombea uongozi tena licha ya kujua anavunja
katiba.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.