Ni marudio ya fainali ya mwaka jana Argentina
watakapocheza dhidi ya Chile kwenye fainali ya Copa America ya 2016
uwanja wa MetLife New Jersey
PREVIEW: Argentina vs Chile
Njia kuelekea fainali kwa Argentina mwaka huu imekuwa rahisi kwani wameshinda kila mchezo kati ya mechi zao tano.
Argentina ambao walianza michuano hiyo kwa kuifunga Chile 2-1 waliendelea kwa kuifunga Panama 5-0 na Bolivia 3-0 kumaliza hatua ya makundi wakiwa kileleni.
Waliendeleza ubabe kwa ushindi wa 4-1 dhidi ya Venezuela na kisha Marekani ambao walichezea kichapo cha 4-0 nusu fainali. Kikosi hicho kinachoongozwa na Lionel Messi kimefunga mabao 18 katika michuano na kuruhusu mawili tu. Walianza michuano kwa nguvu na wanataraji kukomesha ukame wao wa miaka 23 wa mataji Jumapili.
Chile walianza kwa kusua-sua katika michuano hii kwa kipigo kutoka kwa Argentina mechi ya kwanza ya makundi lakini walipata ushindi dhidi ya Bolivia na Panama. Pia walijiwekea historia ya kushinda mabao 7-0 dhidi ya Mexico. Katika hatua ya nusu fainali walifanikiwa kuifunga Colombia kutinga fainali za Copa America.
Habari za Argentina
Tata Martino amepata pigo la majeruhi wakati timu yake ikijiandaa kuimaliza Chile Jumapili usiku kwa majira ya Marekani.
Angel Di Maria ni miongoni mwa wachezaji walio shakani kucheza fainali hiyo wakati Ezequiel Lavezzi akiwa na hitilafu katika mfupa wa mkono. Nicola Gaitan yupo tayari kwa mchezo baada ya kukosa mechi moja kama sehemu ya adhabu lakini hayuko fiti kisawa-sawa. Erik Lamela huenda akaanza, lakini Martino huenda akaamua kumtumia Sergio Aguero pia.
Kikosi cha Argentina (4-3-3)
Romero – Rojo, Funes Mori, Otamendi, Mercado – Mascherano, Banega, Biglia – Lamela, Messi, Higuain.
Habari za timu ya Chile:
Juan Antonio Pizzi amekuwa akibadili kikosi chake katika kila mechi ya hatua ya mtoano na anatarajia kufanya hivyo kuidhibiti safu ya mashambulizi ya Argentina.
Chile kwa sasa hawana matatizo ya majeruhi na kocha wao ana uwanja mpana wa kufanya maamuzi.
Kikosi cha Chile (4-3-3):
Bravo – Beausejour, Jara, Medel, Isla – Vidal, Diaz, Aranguiz – Fuenzalida, Sanchez, Vargas.
Historia ya kukutana Argentina na Chile
Katika fainali za Copa America 2015 Chile walikuwa mabingwa kwa mikwaju ya penalti. Timu hizo zimekutana mara mbili baada ya hapo, na mechi ya hivi karibuni ni ile ya hatua ya makundi Chile waliyofungwa 2-1 na Argentina.
Chile hawajawahi kuifunga Argentina ndani ya dakika 90 katika mechi tano za mwisho walizo kutana Argentina ikishinda mara nne.
Timu hizo zimekutana mara nne kwenye michuano ya Copa America, Argentina wakishinda mechi tatu kati ya hizo, na mechi pekee waliyopoteza ilikuwa fainali ya mwaka jana.
Kwa ujumla Argentina wameshinda mechi 12 kati ya 20 walizowahi kukutana kipindi chote, Chile ikishinda 4 na nyingine 4 zikiwa sare.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.