STAR WA USWIS AFANANISHA JEZI ZAO NA CONDOM
-Puma ambao ni watengenezaji wa jezi za Uswis imesema, wachezaji wa timu hiyo walivaa jezi zilizokuwa na mapungufu ndiyo maana zilikuwa zikichanika wakati wa mchezo wao wa Jumapili dhidi ya Ufaransa uliomalizika kwa suluhu.
Tatizo hilo lilipelekea star wa Uswis Xherdan Shaqiri kusema: “Nadhani Puma hawatengenezi condom.”
Kiungo mpya wa Arsenal Granit Xhaka alilazimika kubadili jezi mara mbili, wakati Valon Behrami, Admir Mehmedi, Fabian Schar, Breel Embolo na Blerim Dzemaili wao wakibadilisha mara moja baada ya jezi zao kuchanika wakati wa mchezo dhidi ya Ufaransa
Kabla ya michuano hiyo kuanza, mshambuliaji Embolo alilazimika kubadili jezi kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Montenegro, wakati mshambuliaji huyo wa Basel akasema: “Tumekuwa na tatizo la jezi. Kit manager wetu bado hajaliona hilo, lakini sisi tumeshaliona.”
Taarifa ya Puma kuomba radhi kwa chama cha soka sha Uswis pamoja na wachezaji ilisema: “hatukutarajia kitu kama hiki.”
Puma wamesema, tatizo hilo limeathiri baadhi ya jezitu, ambazo zilichanganywa na elastane na polyester fibers zilizotengenezwa Uturuki.
Puma wanazalisha jezi kwa nchi tano zinazoshiriki michuano ya Euro 2016 huku Italy ikiwemo.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.