Kikosi
cha Medeama SC Kina hali ngumu ya ukata inayowakabili. Inaonekana mambo
ni magumu hadi sasa hawana uhakika wa kufika Lubumbashi nchini DR Congo
ili kuwavaa TP Mazembe Juni 19.
Katika michuano ya Kombe la Shirikisho, Medeama ya Ghana iko katika kundi moja pia na Yanga na Mo Bejaia.
Imeelezwa
Medema wamekuwa wakifanya kila juhudi kupata fedha lakini wamegonga
mamba na huenda fedha kutoka Shirikisho la Soka Afrika (Caf) ndiyo
zimebaki kuwa tegemeo kwao.
Kawaida
Caf hutoa kiasi cha fedha kwa kila hatua ya michuano hiyo na Medeama
wanaitegemea fedha hiyo ingawa wanaonekana kuwa na wakati mgumu katika
suala la maandalizi.
Hata
hivyo, bado habari hizo hazijathibitishwa na msemaji au ofisa wa juu wa
klabu hiyo. Ingawa ilielezwa mmoja wa viongozi wake, Benjamin Kessie.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.