Kikosi cha Yanga, kipo tayari na kesho kinaondoka mjini Antalya kwenda Algeria kuivaa Mo Bejaia.
Yanga ndiyo timu pekee ya Afrika Mashariki kuingia katika hatua ya Kombe la Shirikisho katika hatua ya robo fainali.
"Kweli
kikosi kinaondoka kesho kwenda Algeria tayari kwa ajili ya mechi hiyo
dhidi ya Mo Bejaia," alisema Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano,
Jerry Muro.
Yanga
ilikuwa kambini Uturuki kwa siku tano kujiandaa na mechi hiyo ya kwanza
ya Kombe la Shirikisho hatua ya robo fainali itakayopigwa Jumapili.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.