Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga, sasa wanarejea nyumbani moja kwa moja kuja kuanza maandalizi ya mechi inayofuata.
Awali
Yanga ilitangaza kuweka kambi nchini Uturuki ili kujiandaa na mechi
yake inayofuata ya Kombe la Shirikisho dhidi ya TP Mazembe.
Lakini
Msemaji na Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro
amesema kikosi hicho kitawasili kesho nchini kikitokea nchini Algeria
ambako kilikwenda kucheza dhidi ya Mo Bejaia na kupoteza kwa bao 1-0.
“Kikosi
kitawasili kesho, tunaamini TP Mazembe ni timu bora lakini tuna uhakika
wa mtaji mkubwa wa mashabiki na pia kikosi bora, tutapambana,” alisema
Muro.
Kabla
ya kucheza Algeria, Yanga iliweka kambi nchini Uturuki kwa siku tano na
kufanya mazoezi ambayo huenda yalisaidia kwa kiasi kikubwa kiuchezaji
kwani katika mechi dhidi ya Bejaia, Yanga ilionyesha soka safi lakini
ikashindwa kuzitumia ili kupata mabao.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.