Wakati
suala la mshambuliaji Mbwana Samatta kuwa njiani kutua AS Roma ya
Italia likiendelea kusambaa mitandaoni, meneja wake amesema ni uzushi
mtupu.
Jamal
Kisongo ambaye ni meneja na mlezi wa Samatta, amesema hakuna lolote
kuhusiana na hilo na Samatta anaendelea na maandalizi katika kikosi
chake cha KRC Genk kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Ubelgiji.
“Nimesikia pia, kuna watu kadhaa wameniuliza pia. Lakini ukweli ni hivi; Mbwana anaendelea na maandalizi ya Ligi Kuu Ubelgiji.
“Hakuna lolote kuhusiana na Roma hadi sasa labda kama litakuja baadaye. Mawakala wake wote wanalijua hilo.
“Timu
haiwezi ikafanya mawasiliano ya kumuuza bila ya kuwaeleza mawakala
wake, meneja wake. Ndiyo maana nasema labda suala hilo lije baadaye,”
alisema Kisongo.
Kuanzia
leo asubuhi, taarifa za AS Roma ya Italia imekuwa kwenye mazungumzo
Genk namna ya kumnasa Samatta ambaye ni nahodha wa taifa Stars, zimekuwa
zikisambaa kwa kasi.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.