Mshambuliaji wa Boca Juniors Carlos Tevez amethibisha kupokea simu kutoka kwa Antonio Conte akitaka kusajili kwenye klabu ya Chelsea.
Star huyo wa zamani wa EPL mwenye miaka 32, kikosi chake cha Boca Juniors kilipoteza mchezo wa fainali ya Copa Libertadores mapema mwezi huu kwa kichapo cha aggregate ya magoli 5-3 dhidi ya Independiente del Valle.
Tevez ameweka wazi kwamba anataka kustaafu soka lake akiwa Boca Juniors na alikiambia kituo cha Radio La Red kwamba, amekataa offer ya Antonio Conte.
“Siku moja baada ya kupoteza mchezo wetu wa fainali, Antonio Conte alinipigia na kuniuliza kama ningependa kujiunga na Chelsea. Nikamwambia hapana.”
Tevez pia akasema siku moja angependa kuwa rais wa klabu ya Boca Juniors.
Kocha wa Chelsea Antonio Conte alitaka kuungana na striker huyo wa Argentina baada ya wawili hao kupata mafanikio pamoja kwenye klabu ya Juvenus.
Carlos Tevez angeongeza uzoefu wake kwenye safu ya ushambuliaji ya The Blues kwasababu alishawahi kucheza kwenye vilabu kadhaa vya Premier League lakini mkongwe huyo hana mpango wa kurudi tena Ulaya.
Amewahi kuvitumikia vilabu vya West Ham United, Manchester United pamoja na Manchester City wakati akicheza soka England.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.