Mamlaka ya soka nchini Uturuki chini ya chama cha soka cha nchi hiyo (TFF) kimeamua kuwafukuza kazi viongozi wa soka nchini humo wakiwemo waamuzi ambao idadi yao inafikia 94.
taarif zinasema kuwa maamuzi hayo yamefikiwa baada ya watu hawa kuonekana ama kuthibitika kuwa walihusika moja kwa moja na majaribio ya mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea nchini humo katika siku za karibuni.
Chama cha soka nchini Uturuki, Turkish Football Federation (TFF) kimetoa taarifa kuwa watu hawa wamefahamika kuhusika katika jaribio la kuipindua serikali lililotokea Julai 15 mwaka huu, ambapo kikundi cha wanajeshi kilitaka kumwondoa madarakani Rais wa nchi hiyo Recep Tayyip Erdogan.
Viongozi wengi waliokuwa chini ya TFF walijiudhuru wikiendi iliyopita kupisha uchunguzi wa kiusalama kujaribu kutizama uwezekano wa watu waliokuwa kwenye mapinduzi hayo maarufu kama Gulen Movement.
Pamoja na hayo, Rais wa TFF, Yildirim Demiroren ameweka wazi kuwa mashindano mbalimbali kama Super Lig, mechi za kimataifa na mashindano mabalimbali yataendelea kama ilivyoelekezwa kwenye ratiba.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.