MTANZANIA ANAECHEZA ZAMBIA AMEITAJA SABABU YA JINA LAKE KUONDOLEWA KIKOSI CHA KWANZA ZESCO V AL AHLY



Na Baraka Mbolembole
MSHAMBULIZI Mtanzania anayekipiga katika timu ya Zesco United ya Zambia leo Jumanne anaweza kufahamu hatima yake kuhusu kushiriki katika kampeni ya timu yake katika Caf Champions League 2016.
Mshambulizi huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar alipangwa katika kikosi cha kwanza wakati Zesco ilipowachapa Al Ahly katika mchezo wa kwanza mwezi Juni kabla ya jina lake kuondolewa baada ya kocha kuambiwa kuwa Mtanzania huyo hajapewa ruhusa na Shirikisho la soka Afrika-CAF.
Jina la Liuzio liliongezwa mara baada ya mchezaji huyo kupona maumivu ya nyama yaliyompata Disemba, 2015 na kuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi minne.
“Najisikia vibaya kwa kweli, timu kucheza CAF bila msaada wangu. Hata kocha nilishamwambia kuhusu hili lakini naye hajuwa akifahamu awali ndiyo maana hata katika game dhidi ya Al Ahly alinipanga katika timu ya kwanza.”
“Ni michuano mikubwa ambayo nina hamu ya kucheza kwa maana timu kubwa zimekuwa zikiitupia macho. Leo nategemea kukutana na meneja ili kujua nini kitafuata. Walichelewa kupeleka jina langu CAF kwa hofu labda nisingekuwa nimepona na kuwa imara kwa michuano,” anasema Liuzio nilipofanya naye mahojiano hii akiwa nchini Zambia.
“Kwa sasa ligi kuu imesimama kupisha kambi ya timu ya Taifa na tupo (Zesco) katika nafasi ya nne lakini tukiwa na michezo minne ya viporo ligi ikiwa mzunguko wa 16,” anasema mshambuliaji huyo mwenye nguvu.
Zesco imekusanya alama 7 katika game zake 4 za dhidi ya Al Ahly, Wydad Casablanca na ASEC Mimosas na inaweza kufuzu kwa nusu fainali ikiwa itamaliza miongoni mwa nafasi mbili za juu katika kundi la kwanza.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.