KRC Genk imeitwanga Westerlo kwa mabao 2-1 katika mechi ya Ligi Kuu ya Ubelgiji.
Mtanzania Mbwana Samatta aliingia katika dakika ya 67 kuchukua nafasi ya Nikos Karelis aliyefunga bao la ushindi katika dakika ya 66.
Samatta hakufunga wala kutoa pasi ya bao katika mechi hiyo, lakini alikuwa msaada mkubwa kuhakikisha wanalinda ushindi wao huo wa nyumbani.
Mara nyingi alikuwa akiwasumbua mabeki wa Westerlo na kusababisha kushindwa kupandisha mashambulizi upande wa Genk.
Alejandro Pozuelo alifunga bao la kwanza la Genk katika dakika ya 54 na Jarno Molenberghs ndiye alifunga lile la kufutia machozi kwa Westerlo..
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.