Mara kadhaa tumesikia wachezaji wakisakamwa na baadhi ya viongozi wakati mwingine mashabiki wao kwamba wanafanya mapenzi mara kwa mara kitu ambacho kinapelekea kuporomoka kwa viwango vyao kiuchezaji wawapo uwanjani.
Ili kupata uthibitisho wa kisayansi, kama kuna uhusiano wowote wa mchezaji kufanya mapenzi mara kwa mara na kudorora kwa kiwango chake, Dkt. Yomba ametoa ufafanuzi kuhusiana na wachezaji na ufanyaji mapenzi mara kwa mara, kuna faida au hasara gani kwa mchezaji kushiriki tendo hilo.
“Kimsingi inaweza ikaleta athari au isilete athari ikawa ni faida, inapokuwa zaidi inaweza ikaleta, madhara lakini inapokuwa kidogo inakuwa na faida mara mbili,” anathibitisha Dkt. Yomba kwa kusema inategemea na mtu atafanya mapenzi kwa kiwango gani.
“Katika mwili wa binadamu kuna kitu kinaitwa hormone, hii ni aina ya vimeng’enywa ambavyo vinakuwepo mwilini, vinasababisha vichocheo katika kazi mbalimbali mwilini. Kuna kitu kinaitwa testosterone , hiki ni kimeng’enyo kwa mwanaume mara nyingi kinapatikana kwenye ‘kende’ zake, kwa mwanamke kinapatikana kwenye mayai (ovaries) lakini kwa kidogo sana huwa kinapatikana kwenye figo.”
“Kinazalishwa kwa wingi kisha kinaingia kwenye damu ambapo inakuwa rahisi kwacho kuzunguka mwilini, kwahiyo hiki kimeng’enyo kinapozaliwa kinapita mpaka kwenye upongo kupitia damu, kinaboreshwa na kina kazi nyingi sana kwa mwanaume na mwanamke, lakini kazi moja wapo ni kujenga misuli yaani kinaimarisha misuli na kufanya mifupa kuwa imara.”
“Kwahiyo kama testosterone ikiwa nyingi kazi yake kubwa ni kusaidia kujenga misuli na kuimarisha mifupa, kwa mchezaji akiwa na vitu hivi viwili basi inamaana vitamsaidia anapokuwa uwanjani kama misuli yake inakuwa imejengeka na mifupa yake inakuwa imara basi inamsaidia.
“Kwanini nimeanza kwanza kuielezea hii hormone, nimeielezea kwasababu wanasayansi wanasema, kufanya mapenzi (tendo la ndoa) ina-boost hiyo hormone kuzalishwa kwa wingi. Kwa maana hiyo ikiwa inazaliwa kwa wingi, inaenda kuleta uimara wa nyama na misuli pamoja na kuipa nguvu miguu.”
“Kwa kuangalia kazi hiyo, kwamba inapozaliwa kwa wingi inaenda kuimarisha misuli, basi inaleta maana kwa mchezaji kwamba kama atashiriki mapenzi kwa sababu hiyo, inaweza ikamuimarisha kwa kumpa nguvu katika misuli yake na kuimarisha miguu. Kwahiyo hapo tunaiona faida kwasababu nimeshaeleza umuhimu wake na kazi yake kubwa mwilini ni nini.”
“Hizi faida utazipata vizuri zaidi kwa kupata nafasi ya kushiriki kwa mtu wako kama ni mkeo au mpenzi wako na unatakiwa kuamini kabisa kufanya mapenzi kabla ya mechi haiwezi kuathiri performance, badala yake uta-perform zaidi.”
Mchezaji wa zamani wa Brazil Ronaldo de Lima aliwahi kuweka wazi kwamba, yeye hupenda kufanya tendo la ndoa kabla ya mechi hususan mechi kubwa akisema huwa inamfanya kuwa na nguvu ya kupambana dhidi ya timu anayokutana nayo.
SOURCE SHAFIH DAUDA
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.