Mkurugenzi
wa Kampuni ya Millen Magese Group (MMG), Millen Magese ameishukuru
Serikali kupitia kwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape
Nnauye, huku akifurahishwa na uwakilishi mzuri wa Miss Tanzania Julitha
Kabete (19), aliyeingia kwenye tano bora katika mashindano ya Afrika.
Kabete alipeperusha
vema Bendera ya Tanzania kwa kuingia hatua ya tano bora ya mashindano
yaliyofanyika Jumamosi nchini Nigeria na kuitoa Tanzania kimasomaso.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Millen alisema ni faraja kubwa kwake na nchi
yake kwa Julitha kuingia hatua ya tano bora, lakini sababu kubwa ikiwa
ni ushirikiano iliyoupata.
"Napenda
kuchukua fursa hii kwa heshima nyingi na taadhima kuishukuru Serikali
ya Awamu ya Tano kwa ushirikiano wa hali ya juu, kupitia Waziri Nape
Nnauye kwa ushirikiano na mwongozo wa kipekee, wazazi na familia nzima
ya Julitha kwa malezi yenu kwa binti , Kamati nzima ya Miss Tanzania
chini ya Mkurugenzi Hashim Lundenga (Tunashukuru sana), kwenu wanahabari
hatuna maneno sahihi ya shukrani, asanteni sana," alisema Magese.
Naye
mshindi huyo wa tano wa Miss Afrika, Julitha Kabete, alisema anashukuru
kwa ushirikiano aliupata, lakini pia nchi yake kupata thamani ya
kipekee katika shindano hilo kupata nafasi tano za juu.
Kabete
alisema kuwa licha kutopata nafasi ya kwanza, lakini ameweza
kuiwakilisha vema nchi katika shindano hilo, kwa sababu ushindani
ulikuwa mkali sana.
"Kwangu
ni faraja kubwa kwa kuwa balozi mzuri wa Tanzania na kuweza kuwashinda
wenzangu wengi ikiwemo na mwenyeji wetu ambaye hakuingia katika hatua ya
tano kama ambayo mimi nimeipata nina furaha kubwa sana,"alisema
Kabete.
Alisema
kuna mkataba mpya ambao utaingiwa kati ya Tanzania na waandaaji wa
shindano hilo la Miss Africa katika kutoa ushirikiano wa ushiriki wa
shindano hilo.
Katika
shindano hilo lililofanyika Novemba 26, mwaka huu nchini Nigeria, taji
la shindano hilo lilienda kwa mnyange Neurite Mendes (23) wa Angola,
aliyenyakua kitita cha dola za Marekani 25,000 sawa na sh.milioni 52 ya
Kitanzania na gari jipya (brand new 2016 Ford Escape), safari maalum ya
mafunzo nchini Uingereza na Ubalozi wa Mazingira– Afrika.
Mshindi
wa pili katika shindano hilo ni Refilwe Mthimunye wa Afrika Kusini
alipata dola za Kimarekani 15, 000 ni sawa na zaidi ya sh. milioni 32,
na Jencey Anwifoje kutoka nchini Cameroon, akiibuka wa tatu na kupata
dola za kimarekani 10,000 sawa na zaidi ya sh.milioni 20.
Shindano
la Miss Afrika 2016 lilichagizwa kwa heshima ya mji wa Calabar na jimbo
la Cross River, chini ya Gavana wa Cross River Profesa Ben Ayade.
Kampuni
tanzu ya Millen Magese (MMG) imeanzishwa kwalengo la kuibua, kuinua,
kutambua na kukuza vipaji katika Bara la Afrika na ngazi ya Kimataifa.
MMG
imeweza kufika nchi mbalimbali barani Afrika na mwaka 2012 iliweza
kuendesha shindano la kwanza ya aina yake ambapo wanamitindo wawili
kutoka Tanzania walipata nafasi ya kupata mikataba nchini Afrika
Kusini.
Wanamitindo
kutoka mashindano hayo wameweza kuendelea kufanya vizuri maonesho
mbalimbali ya kitaifa na kimataifa. Mwaka huo huo wa 2012 MMG kupitia
mradi wa TIFEX iliwezesha wabunifu kutoka nchini kupata uzoefu na uelewa
wa wiki za mitindo duniani.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.