GHANA,MISRI,CAMEROON NA BURKINAFASO HIZOOOOOO NUSU FAINALI AFCON





Andre Ayew na mdogo wake, Jordan Ayew kila mmoja amefunga bao moja na kuisaidia Ghana kuifunga DR Congo kwa mabao 2-1 katika mechi ya robo fainali ya michuano ya Afcon nchini Gabon.

Jordan ndiye alianza kufunga dakika ya 63 na kaka yake akamalizia kazi katika dakika ya 78 kwa mkwaju wa penalti.

Wote wawili ni watoto wa gwiji la soka nchini Ghana Abeid Ayew maarufu kama Abeid Pele.

Michezo mingine ya robo fainali ya kombe hilo la AFCON Burkinafaso waliifunga Tunisia Magoli 2-0 Misri ikishinda 1-0 dhidi ya morocco huku Senegal ikitolewa kwa changamoto za mikwaju ya penalty 5-4 dhidi ya Cameroon baada ya dk 120 kumalizika bila kufungana.

Kwa matokeo hayo sasa michuano hiyo inatinga hatua ya nusu fainali ambapo nusu fainali ya kwanza ni tarehe 1 mwezi wa pili itakazozikutanisha timu za Burkinafaso dhidi ya Misri huku nusu fainal ya pili ikipigwaa tarehe 2 mwezi wa pili Cameroon dhidi ya Ghana.

Fainali ya michuano hiyo itapigwa tarehe 5 ya mwezi wa pili kati ya timu mbili zitakazoshinda katika michezo yao ya nusu fainali itakayopigwa mapema mwezi wa pili.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.