VIDEO-LEBRON JAMES MCHEZAJI BORA ZAIDI KATIKA MPIRA WA KIKAPU WA CLEVELAND CAVALIERS

Mchezaji bora zaidi katika mpira wa kikapu kuwa ni LeBron James wa Cleveland Cavaliers. 

NA SALEH ALLY 
KWA sasa hakuna ubishi mchezaji bora zaidi katika mpira wa kikapu kuwa ni LeBron James wa Cleveland Cavaliers. Katika fainali za NBA za msimu uliopita, LeBron alifanya kazi ya ziada kuiongoza Cavaliers kuibuka mabingwa dhidi ya kikosi cha Golden State Warriors kilichokuwa kinapewa nafasi kubwa.  
LeBron akabadili mambo na kuweka rekodi kibao huku akiwa amefunga pointi nyingi na kutoa pasi ny- ingi zaidi zilizoitengeneza timu hiyo na kuwa bora katika ushambulizi.  
Katika fainali za msimu huu, kwa mara nyingine Cavaliers wanakutana tena na Warriors na tayari zimeshachezwa mechi mbili, zote Cavaliers wamepoteza na kufanya matokeo hadi sasa kuwa 2-0. Cavaliers wanaendelea kubaki na LeBron lakini Warriors wao wanajivunia Stephen Curry ambaye walikuwa naye msimu uliopita kwa kuwa ndiye nyota wao.Mgeni katika Golden State ni Kevin Durant ambaye mashabiki wengi wa mpira wa kikapu wanapenda kumuita KD. Durant alikuwa katika kikosi cha Oklahoma City Thunders pamoja na Mtanzania Hasheem Thabeet. Mwisho amekuwa ndiye tegemeo wa kikosi hicho kabla ya kuhamia Warriors. Mashabiki wa Warriors wanaposikia Durant ni majeruhi au mgonjwa, hofu inatawala.  
Hii inatokana na mchango ambao ameuonyesha na umezaa imani kubwa wa mchango wake unafanya W a r r i o r s waamini Curry peke yake bila ya yeye mambo yatakuwa magumu. Hivyo nguvu ya Curry sasa inaegemea kwake na amegeuka kuwa dereva wa timu kwa kuthibitisha ubora wake. Katika mechi ya pili dhidi ya Cavs, Durant aliiongoza timu yake kushinda kwa pointi 132113, lakini mchango wake ulikuwa mkubwa zaidi katika kuendesha timu, kuzuia na kufunga. Takwimu zinaonyesha alicheza dakika 41 ambazo ni nyingi, akatoa asisti 6, akablock mara 5, rebaundi 13 na kufunga pointi 33.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.