KOCHA WA ZAMANI WA UINGEREZA MBIONI KUINOA CAMEROON....



Cameroon imethibitisha kufanya mazungumzo na kocha wa zamani wa England Sven-Goran Eriksson kuchukua usukani wa kuifunza timu ya taifa hilo Indomitable Lions.
Eriksson mwenye umri wa miaka , 70, raia wa Sweden alikuwa na mazungumzo mazuri na maafisa wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Cameroon (Fecafoot) mjini Yaoundé wiki iliyopita waliokuwa wakitaka kuziba pengo lililoachwa baada ya kuondoka kwa Hugo Broos.
"Baada ya kukaa saa 72, Sven-Goran Eriksson aliondoka Yaoundé Jumamosi tarehe 28 July 2018," Fecafool lilieleza kwenye ukurasa wake wa Twitter.
" Meneja huyo raia wa Sweden alikuwa amekaribishwa na Cameroon kwa mazungumzo juu ya kuajiriwa kwa kocha mkuu wa timu kuu ya taifa - the Indomitable Lions.
" Baada ya kumpa mtihani wa kazi Sven-Goran Eriksson na kuzingatia mapendekezo mengine yaliyopo, Fecafoot litafichua chaguo lake la kocha wa kudumu wa timu yetu ya taifa lilieleza shirikisho hilo la mpira wa miguu la Cameroon.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.