Yannick
Ferreira Carrasco ni raia wa Ubelgiji, ana miaka 22 tu, ndiye alifunga
bao la Atletico Madrid katika dakika za mwisho na kuikoa na kipigo cha
ndani ya dakika 90 dhidi ya wapinzani wao wakubwa Real Madrid katika
fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Carrasso
ambaye mzazi wake mmoja ni Mbelgiji na mmoja ni Mhispania ni kati ya
wachezaji wa timu ya taifa ya Ubelgiji pia ni kati ya wachezaji vijana
waliopita hatua zote kwa ubora wa juu.
Moja
ya timu alizopitia ni Genk ambayo sasa anaichezea mshambuliaji
Mtanzania Mbwana Samatta, baada ya hapo akapelekwa Monaco B ya Ufaransa
katika kupandishwa katika timu ya wakubwa ya Monaco 2012 hadi 2015 yaani
mwaka jana alipojiunga na Atletico Madrid.
Ameichezea
Atletico Madrid mechi 29 akiwa amefunga mabao 5 kabla ya Kocha Diego
Simeone kumuamini leo na kumpa nafasi ya kucheza katika mechi hiyo kubwa
kuliko zote katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Anaaminika
kuwa mmoja wa viungo washambuliaji wenye uwezo wa juu kabisa katika
bara la Ulaya baada ya miaka miwili au mitatu ijayo kama ataendelea
kudumisha kiwango chake.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.