Baraza
la wazee la Yanga wameliomba Baraza la Michezo Tanzania (BMT) na
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwakubalia kutumia kadi mbili za
zamani na za Posta katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo.
Uchaguzi
mkuu wa Yanga umepangwa kufanyika Mei 27, mwaka huu na Kamati ya TFF
imetangaza uchaguzi huo juzi ilitangaza jana ndiyo siku ya kuanza kutoa
fomu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Katibu
wa baraza la wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali amesema kama kuna baadhi
watapiga kura na wengine kuachwa, haitakuwa sawasawa.
"Kama wengine watapiga wakiwa na kadi za zamani ana kuwaacha wale wenye kadi za uanachama za benki ya Posta, haitakuwa sawa.
"Wako
waliokuwa wana kadi za zamani, wakabadili na kuchukua zile za Posta.
Wengine kweli ni wapya, sasa kuwaacha wengine na wengine wapige ni
kuleta mgogoro," alisema Akilimali.
Pia baraza hilo limeomba BMT na TFF kuitishwa mkutano wa dharura wa klabu hiyo ambao utahusiana na masuala ya uchaguzi.
"Pia
ninaomba kama watakubali katika mkutano huo pia wawashirikishe watu
kutoka wizara ya michezo, viongozi wa Chama cha Soka Dar es Salaam
(DRFA)," alisema.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.