Siku
chache baada ya Patrick Kahemele kutua ndani ya Klabu ya Simba na
kukabidhiwa cho cha ukatibu mkuu, ameibuka na kuweka wazi mipango mipya
kwa ajili ya kuisuka Simba ya msimu ujao.
Kahemele
ambaye awali aliwahi kuwa Meneja wa Azam FC, ameeleza kufurahi kujiunga
na Simba na kusema kwa pamoja atashirikiana na viongozi wenzake kuweka
sawa mambo na kuifanya Simba kuwa tishio msimu ujao.
Akizungumza
hivi karibuni jijini Dar, Kahemele alisema anatambua jinsi gani Simba
imekuwa na kiu ya makombe kwa miaka minne sasa na kwamba katika utendaji
wake ameahidi mapema ataanza na hilo kisha kuijenga Simba itakayokuwa
na njia sahihi za kujitegemea yenyewe kujiendesha bila kuhitaji msaada
kwa mtu binafsi.
“Kuna
mengi ya kufanya kwa ajili ya kuiweka sawa zaidi Simba, natambua kuna
hili la makombe, mashabiki wamekikosa hicho kitu kwa muda sasa,
tunahitaji kikosi kikali na cha ushindani mkubwa msimu ujao pamoja na
mambo mengi ikiwemo kuiweka Simba sehemu sahihi ya kujiendesha yenyewe.
“Haya
yote kwa kushirikiana na uongozi naamini yatafanikiwa na Simba itakuwa
kwenye mstari wake kwa mara nyingine tena, zaidi nashukuru kwanza nipo
kwa mashabiki ambao watulivu, hawana tatizo na wanaelewa mambo ya soka
yanavyokwenda,” alisema Kahemele.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.