Mkuu
wa kitengo cha habari cha klabu ya Yanga, Jerry Muro ndiye mgeni rasmi
wa mechi ya Kombe la Shirikisho kati ya Yanga dhidi ya TP Mazembe.
Mechi
hiyo inayosubiriwa kwa hamu, itapigwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam na tayari Yanga wametangaza mchezo huo ni bure,
yaani mashabiki hawatalipa kiingilio.
Taarifa
za ndani kutoka Yanga zinaeleza kuwa Muro ndiye atakuwa mgeni rasmi na
kama kutakuwa na mgeni kutoka serikalini, Muro atabaki kuwa mgeni rasmi
upande wa Yanga.
“Kweli hilo limepitishwa, Muro atakuwa mgeni rasmi,” kilieleza chanzo cha uhakika.
Juhudi za kumpata Muro kulizungumzia suala hilo, kuligonga mwamba kwa kuwa hakupokoea simu yake ya mkononi.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.