Shirikisho
la Soka la Afrika (Caf) limetoa ufafanuzi kuhusiana na beki wa Yanga,
Hassan Kessy kuhusu mechi ya kesho ya Kombe la Shirikisho kati ya Yanga
dhidi ya Mo Bejaia ya Algeria.
Awali,
shirikisho hilo, lilieleza kuhusiana na suala la Kessy kulazimika kuwa
na barua ya ruhusa kutoka Simba kwa kuwa ni klabu aliyotoka.
Lakini
Msemaji wa Caf, Junior Binyam amesema kinachotakiwa kufuatwa katika
hili ni Yanga kuangalia kama wamekamilisha taratibu za usajili za
michuano ya Kombe la Shirikisho.
“Suala
la kama hakuna malalamiko katika klabu anayotokea ni muhimu sana, baada
ya hapo ni kuangalia kama usajili wa michuano hiyo umefuatwa. Kuna aina
mbili, kwenye mtandao na kawaida.
“Kama
Caf imetoa leseni, kunakuwa hakuna shida. Lakini kunaweza kuwa na
angalizo la kuangalia kama mchezaji hana mkataba tena na klabu
aliyotokea au walimalizana kwa kufuata taratibu zote.
“Kama
atakuwa amemaliza mkataba na klabu aliyotokea, hakika hakuna tatizo
hata kidogo na linaloangaliwa hapo ni hivi; usajili wa Caf umekamilika?
Leseni imetoka? Kama hayo yametekelezwa, hakuna tatizo,” alisema.
Alipotafutwa
mara ya pili kuhusiana na suala la Kessy, Binyam alisema: “Nimeambiwa
Yanga wamezungumza na wenzetu wakati wa pre-match meeting kule Algeria,
wameuliza maswali yote na kujibiwa vizuri na wameelewa.
“Ninaamini
wachezaji wao watakuwa hawana tatizo kwa maana ya usajili wa Caf.
Kwenye suala la usajili katika klabu walizotoka, hili tunaweza kusubiri
chama cha nchi yenu (TFF) ndiyo waseme. Lakini hadi sasa, inaonekana
wachezaji hao wanaweza kutumika, hilo tuwaachie wao (Yanga).”
Kwa
kauli hiyo inaonekana Yanga, wana kila sababu ya kuwatumia Kessy, Juma
Mahadhi, Adnrew Vicent ‘Dante’ na Beno Kakolanya ambao wamesajiliwa.
Lakini Obey Chirwa raia wa Zambia atalazimika kusubiri wakati Yanga
ikipambana kumtafutia usajili wake wa leseni kutoka Caf.
HIZI NI SEHEMU YA SHERIA ZA USAJILI WA MICHUANO YA KOMBE LA SHIRIKISHO NA KLABU INATAKIWA KUFANYA NINI KUKAMILISHA USAJILI WA MCHEZAJI AMBAZO UFAFANUZI WA BINYAM UNAPITIA HUMU. |
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.