GIROUD, PAYET WAIBEBA UFARANSA MECHI YA KWANZA EURO IKIITWANGA ROMANIA 2-1



Ufaransa imefanikiwa kuanza vizuri michuano ya Euro 2016 ikiwa mwenyeji baada ya kuifunga timu ngumu ya Romania kwa mabao 2-1.

Huo ndiyo ulikuwa mchezo wa kwanza au wa ufunguzi wa michuano hiyo itakayochezwa nchini Ufaransa.

Ufaransa ilianza kupata bao kupitia mshambuliaji Olvier Giroud wa Arsenal, ambaye aliunganisha krosi nzuri ya Dimitr Payet mwanzoni mwa kipindi cha pili.

Romania walipata penati kutokana na Patrice Evra kumuangusha Stancu na wakasawazisha lakini Payet anayekipiga West Ham akaachia bunduki katika dakika ya 88 iliyozaa bao la pili na la ushindi.

Ufaransa imefanikiwa kuanza vizuri huku Payet na Paul Pogba waking’ara, hata hivbyo ,haikuwa mechi rahisi kwao.








Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.