Mourinho anaripotiwa kumuona Pogba kama tofali lake la kwanza la kuijenga upya Man United, japokuwa Pogba aliondoka bure United miaka 4 iliyopita.
Ofa ya United ina malipo ya aina awamu mbili, awamu ya kwanza watalipa kiasi cha £48m na kinachobaki cha £12m kitakuwa viongezeko ambavyo United watavilipa kutokana na mafanikio ya Pogba katika uwepo wake ndani ya kikosi cha Mourinho.
Viongezeko hivyo vitalifanya dili kufikia kiasi cha £59.7m, kiasi cha fedha walicholipa United kwa ajili ya kumsaini Angel Di Maria in 2014.
Mabingwa wa Italia bado hawajajibu ofa ya United, lakini kadri siku zinavyoenda wanaona wazi wapo karibu kumpoteza staa wao.
Pogba amekuwa akitoa kauli za kuonyesha kwamba ameshashinda kila kitu na Juventus na sasa anahitaji changamoto mpya na hivyo kuondoka na option mojawapo.
Inaaminika Pogba ambaye kwasasa yupo nchini Ufaransa na timu yake ya taifa ya nchi hiyo kwa ajili ya Euro 2016 – amemuachia majukumu wakala wake Mino Raiola ambaye amekuwa akisikiliza ofa kutoka klabu mbalimbali kwa miezi takribani mitatu.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.