KALABA |
TP
Mazembe imeanza hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho kwa
kishindo baada ya kutoa kipigo cha mabao 3-1 kwa wageni wake, Medeama
kutoka Ghana.
Medeama
wamekutana na adhabu hiyo mjini Lubumbashi, DR Congo ikiwa ni mechi ya
kwanza kabisa ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho.
Medema
ndiyo walitangulia kupata bao kupitia Malik Okowuah katika dakika ya
nne tu ya mchezo. Hali hiyo ilionekana kuwazindua Mazembe ambao wakaanza
kushambulia mfululizo.
Rainford
Kalaba ndiye alianza kutikisa nyavu za Medeama katika dakika ya 21
kabya ya Salif Coulibaly kuandika bao la pili katika dakika ya 45. Timu
hizo zikaenda mapumziko wenyeji wakiwa wanaongoza kwa idadi hiyo.
Kipindi cha pili kilionekana cha Mazembe wakitawala kila idara hadi Kalaba alipofunga bao la tatu katika dakika ya 73.
Mazembe
na Medeama ziko kundi A ambalo wawakilishi wa Tanzania, Yanga pia wamo
na wanatarajia kucheza dhidi ya Mo Bejaia wakiwa ugenini katika mechi
inayosubiriwa kwa hamu saa chache zijazo.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.