KIUNGO
wa Atletico Madrid, Saul Niguez, anayetakiwa kwa dau la Pauni Milioni
54 na kocha Jose Mourinho wa Manchester United, hajajumuishwa kwenye
kikosi cha mwisho cha Hispania cha Euro 2016.
Kinda
huyo wa umri wa miaka 21, aliyecheza vizuri fainali ya Ligi ya Mabingwa
Ulaya wakifungwa na Real Madrid kwa penalti 5-3 baada ya sare ya 1-1,
ametemwa kwenye kikosi cha mwisho cha Hispania pamoja na Isco.
Baada
ya awali kuteua kikosi cha wachezaji 19, kocha Vicente del Bosque
ametaja wachezaji wanne wa kukamilisha orodha ya wachezaji 23
akiwachukua Sergio Ramos, Juanfran, Lucas Vazquez na Koke - ambaye pia
alicheza fainali ya Ligi ya Mabingwa San Siro Jumamosi.
KIKOSI CHA MWISHO CHA HISPANIA EURO 2016
Makipa: Iker Casillas (Porto), David De Gea (Man United), Sergio Rico (Sevilla)
Mabeki: Sergio
Ramos (Real Madrid), Gerard Pique, Jordi Alba, Marc Bartra (all
Barcelona), Cesar Azpilicueta (Chelsea), Mikel San Jose (Athletic
Bilbao), Hector Bellerin (Arsenal), Juanfran (Atletico Madrid)
Viungo: Bruno
(Villarreal), Sergio Busquets, Andres Iniesta (both Barcelona), Thiago
(Bayern Munich), David Silva (Manchester City), Pedro, Cesc Fabregas
(both Chelsea), Lucas Vazquez (Real Madrid), Koke (Atletico Madrid)
Washambuliaji: Aritz Aduriz (Athletic Bilbao), Nolito (Celta Vigo), Alvaro Morata (Juventus)
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.