Timu
ya taifa ya Misri, Pharaos, inatarajiwa kutua nchini leo Jumatano kwa
ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu Michuano ya Mataifa ya Afrika (Afcon
2017) dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
Mchezo
huo wa Kundi G unatarajiwa kupigwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Taifa
Dar, ambapo utachezeshwa na mwamuzi Meya Bastred akisaidiana na Mihndou
Gauthar na Vinga Theophil na mwamuzi wa mezani ni Oboga Eric, wote
kutoka nchini Gabon.
Katika
kundi hilo Misri ndiyo wanaongoza wakiwa na pointi saba wakifuatiwa na
Nigeria wenye pointi mbili Tanzania ni ya tatu ikiwa na pointi moja,
hivyo inahitaji ushindi ili kuwa na matumaini ya kufuzu.
Msemaji
wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Alfred Lucas, alisema kuwa kwa
asilimia kubwa maandalizi yote ya mchezo huo yamekamilika na wamejipanga
vizuri kuwapokea wageni wao hao.
“Timu
ya Misri watafika kesho (leo) lakini bado hawajatuambia muda gani
watakuja, kila kitu kipo vizuri, huu ni mchezo muhimu kwa Srars kwani
kwa vyovyote vile inatakiwa kupata ushindi kwenye mchezo huo,” alisema
Lucas.
Mbali
na hilo Lucas pia alisema: “Timu yetu ya taifa ya wanawake, Twiga
Stars, inatarajiwa kwenda Kigali, Rwanda kucheza mechi ya kirafiki,
mchezo ambao unatarajiwa kupigwaJune 17 mwaka huu, watautumia mchezo huo
kwa maandalizi ya mechi zao za kuwania kupata nafasi ya kucheza
mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa wanawake hapo mwakani.”
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.