USWIZI WAFUNGUA EURO KWA USHINDI, WAICHAPA ALBANIA 1-0



Albania vs Swiss

Uswizi imefanikiwa kuifunga Albania kwa goli 1-0 katika mchezo kundi A kwenye muendelezo wa michuano ya Euro 2016 inayofanyika nchini Ufaransa. Mchezo huo ulipigwa katika kunako uwanja wa Stade Bollaert-Delelis unaopatikana katika mji wa Lens.

Kona nzuri iliyochongwa na Xherdan Shaqiri na kumshinda kipa wa Albania Etrit Berisha,  na baadaye kumaliziwa kwa umaridadi wa hali ya juu na Fabian Schar kunako dakika ya tano tu ya mchezo, ndiyo iliyowahakikishia ushindi Uswizi katika mchezo wa leo.

Licha ya Uswizi kuonekana wazuri zaidi lakini Armando Sadiku wa Albania alikosa nafasi ya wazi ambayo ingewapa goli la kusawazisha lakini umakini mdogo ndiyo ulimgharimu.
Albania walipata pigo kunako dakika ya 36 baada ya nahodha wao Lorik Cana baada ya kuunawa mpira kwa makusudi na ndipo refarii alipoamua kuchukua maamuzi hayo.

Kwa sasa Uswizi wanashika nafasi ya pili katika kundi A nyuma ya Ufaransa, wakilingana pointi lakini wakizidiwa kwa utofauti wa magoli ya kufunga na kufungwa. Jana Ufaransa waliifunga Romania kwa magoli 2-1.

Hii inawapa viashirio vya kufuzu hatua ya mtoano kwa mara ya kwanza baada ya kumaliza mkiani kwenye michuano ya miaka ya 1996, 2004 na 2008.
Dondoo muhimu
  • Uswizi wameshinda michezo sita kati ya saba ya mwisho waliyokutana na Albania huko mmoja wakitoka sare.
  • Xherdan Shaqiri ametoa mchango ama amehusika kwenye magoli tisa kwa Uswizi katika michezo nane iliyopita ya kimashindano (akifunga magoli matano na kutoa pasi nne za magoli)
  • Timu nne za mwisho ambazo zimepata fursa ya kucheza kwa mara ya kwanza kwenye michuano ya Euro zimepoteza michezo yao (Latvia 2004, Poland na Austria 2008 na Albania 2016)
  • Albania ni timu ya nne ambayo inashiriki kwa mara ya kwanza kwa mchezaji wake kuoneshwa kadi nyekundu katika historia ya michuano ya Euro (England 1968, Netherlands 1976 na Bulgaria 1996).
  • Albania’s Etrit Berisha made six saves in this game, more than he did in any of the Euro 2016 qualifiers.
  • Kipa wa Albania Etrit Berisha ameokoa michomo sita katika mchezo wa leo, zaidi ya aliyookoa katika mchezo wowote kwenye hatua ya awali ya kufuzu michuano hii.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.