MSHAMBULIAJI
wa kimataifa wa England, Jamie Vardy amekubali kusaini Mkataba mpya wa
miaka minne kuendelea kuchezea klabu yake, Leicester City na kukataa ofa
ya kujiunga na Arsenal.
Mustakabali wa mkali huyo wa mabao wa England umekuwa haueleweki tangu Arsene Wenger atangaze ofa ya Pauni Milioni 20 kumnunua Juni 3, mwaka huu, lakini ameipiga chini ofa hiyo na kuamua kubaki Uwanja wa King Power.
Baada ya Arsenal kumpa ya mshahara wa Pauni 120,000 kwa wiki, Leicester City nayo imemuongezea mshahara mchezaji huyo hadi pauni 100,000 kwa wiki na Vardy atasaini Mkataba mpya atakaporejea kutoka kwenye Euro 2016 nchini Ufaransa.
Vardy aliisaidia Leicester City kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya England akifunga jumla ya mabao 24 msimu uliopita
Mbali
ya mshahara mkubwa zaidi, lakini Vardy angenufaika zaidi kwa kipato
Uwanja wa Emirates kutokana na hali nzuri ya kiuchumi na sera za malipo
za Arsenal ukilinganisha na Leicester.
Iwapo
atasaini Mkataba mpya, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 atadumu
King Power hadi mwaka 2020 atakapofikisha umri wa miaka 33 – jambo
ambalo ni habari njema kwa kila mmoja ndani ya Leicester City.
Vardy
alikuwa chachu ya mafanikio ya Leicester City msimu uliopita ikitwaa
ubingwa wa Ligi Kuu ya England, akifunga jumla ya mabao 24.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.