WAKIMATAIFA DHIDI YA TP MAZEMBE MTANANGE JUMANNE SAA KUMI JIONI



Baada ya mvutano kati ya Yanga na Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kwamba mechi ya Kombe la Shirikisho kati ya Yanga dhidi ya TP Mazembe ichezwe lini kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, sasa jibu ni Jumanne.

Msemaji wa TFF, Alfred Lucas ameendelea kusisitiza mechi hiyo itachezwa Jumanne kama ilivyotangazwa awali, na si kama walivyotangaza Yanga 
 
Lakini Yanga kupitia Kurugenzi yao ya Habari na Mawasiliano, Msemaji wao, Jerry Muro amesema: “Ni kweli.”

Muro amesema wamefikia hivyo baada ya kutokuwa na uhakika kama kweli kuna umeme wa uhakika.

“Mechi itachezwa Jumanne na si Jumatano, kuchezwa usiku inaonekana hatuna uhakika wa umeme,” alisema Muro.


“Pia hatuna uhakika wa jenereta, hivyo hatuwezi kuingia kwenye hasara au kujaribisha kitu cha hatari wakati tunajua tunaweza kupoteza pointi kwa kanuni za Caf.”
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.