Kocha Joseph Omog raia wa Cameroon amesaini mkataba wa miaka miwili kuionoa Simba ya Dar es Salaam, mkataba huo utaisha mwaka 2018.
Omog
amesaini mkataba huo leo jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa
habari akiwa pamoja na Rais wa Simba, Evans Elieza Aveva.
Omog
amesema anaujua ukubwa wa Simba na changamoto zake na amesisitiza
atapambana kuhakikisha kunakuwa na mabadiliko ingawa amesisitiza suala
la muda kwa kuwa kila kitu hakiwezi kubadilika siku moja.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.