KASEKE (KULIA)... |
Kiungo mshambuliaji wa Yanga Deus Kaseke jana alinusurika kifo baada ya kupata ajali mbaya jijini Dar.
Kaseke
ambaye alijiunga na Yanga akitokea Mbeya City alipata ajali hiyo akiwa
amepanda pikipiki asubuhi wakati akiwahi mazoezi ya timu hiyo
yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Boko Veterani.
Yanga
inatarajiwa kuvaana na Medeama ya Ghana kwenye michuano ya Kombe la
Shirikisho Afrika mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa Julai 15,
mwaka huu.
Timu
hiyo, tayari imepoteza michezo yake miwili hadi hivi sasa katika hatua
ya makundi ya michuano hiyo dhidi ya MO Bejaia na TP Mazembe ambayo kila
mmoja walifungwa bao 1-0.
Championi
Jumatano, ambalo lilikuwa kwenye mazoezi ya Yanga jana, lilimshuhudia
kiungo huyo akiwa nje ya uwanja akishindwa kufanya mazoezi na wenzake
kutokana na maumivu makali aliyokuwa ameyapata mwilini mwake.
Daktari
mkuu wa timu hiyo, Edward Bavo, alisema beki huyo ameshindwa kufanya
mazoezi na wenzake kutokana na maumivu na majeraha aliyoyapata baada ya
kupata ajali ya bodaboda.
Bavo alisema, kiungo huyo alipata ajali hiyo asubuhi ya jana maeneo ya Ubungo wakati akiwa anakwenda mazoezi Boko.
"Kaseke
ameshindwa kufanya mazoezi baada ya kupata ajali ya bodaboda
iliyomsababishia michubuko kwenye magoti na sehemu nyingine za mwili
wake.
"Ajali
hiyo aliipata maeneo ya Ubungo akiwa anatokea kwake Kimara anapokaa,
hivyo uongozi umemuwahisha hospitali kwa ajili ya matibabu
zaidi,"alisema Bavo.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.