Mabingwa wa ligi
nchini Uingereza Leicester wameingia katika mkataba na klabu ya CSKA
Moscow kumsajili mshambuliaji wa Nigeria Ahmed Musa,kulingana na ajenti
wa mchezaji huyo.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka
23,aliyejiunga na CSKA mwaka 2012 na kufunga mabao 54 katika mechi 168
anatarajiwa kutia saini kile ambacho BBC Sport inasema huenda ikawa
kitita kikubwa zaidi kuwahi kutolewa kwa mchezaji katika klabu hiyo.
''Kila kitu kimefanikishwa na Musa atakuwa nchini Uingereza ili kufanyiwa vipimo vya kimatibabu siku ya Jumatano''.
BBC Sport ina ufahamu kwamba Musa alikataa wito wa Southampton,Everton na West Ham. Mkufunzi wa CSKA Moscow Leonid Slutsky alikiri
kwamba raia huyo wa Nigeria ambaye anaweza kucheza kama winga anakaribia
kuondoka katika klabu hiyo.
''Atandoka siku ya Jumanne'',Slutsky alivambia vyombo vya habari vya Urusi.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
RELATED POSTS
Blogger Comment
0
comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.