Antoine Griezmann na Gareth Bale wanastahili kuingia
kwenye kinyang'anyiro cha Ballon d'Or kwa mujibu wa nyota wa zamani wa
Barcelona Hristo Stoichkov
Griezmann na Bale wanajiandaa kwa mechi za nusu fainali Euro 2016 baada ya kampeni nzuri walizofanya katika klabu zao Atletico na Real Madrid.
Mfaransa Greizmann amefunga mabao 32 katika michuano yote akiwa Atletico timu yake ikimaliza nafasi ya tatu La Liga na kupoteza fainali Ligi ya Mabingwa kwa Real Madrid, wakati Bale akiwa amefunga mara 19 na kutoa pasi 10 za goli.
Lakini ikiwa ni wiki moja tangu alipomtaja James Rodriguez wa Real Madrid kama mchezaji wa kawaida sana, mkongwe huyo wa Bulgaria aliamua kumzungumzia mshindi wa mara nne wa tuzo ya Ballon d'Or Ronaldo.
"Grizemann ni mchezaji hatari kwa kila mtu na anacheza soka matata sana," Stoichkov aliiambia redio ya Hispania Cadena Cope.
"Lakini huenda wakampa Cristiano Ronaldo tuzo hiyo tena kwa sababu ya umbile lake zuri!"
Kuhusu Bale - ambaye atacheza dhidi ya Ureno Alhamisi - hali kadhalika naye akitarajiwa kuingia kwenye mbio za Ballon d'Or, Stoichkov amesema mchawi huyo wa soka wa Wales atakuwa miongoni mwa wanaowania tuzo hiyo iwapoa Wales itatinga fainali EURO.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.