Mmoja
wa watangazaji wa Kituo cha Televisheni cha SuperSport juzi aliutangazia
umma kuwa kiungo wa Zesco, Misheck Chaila, anakwenda Simba.
Kiungo
huyo amekuwa akitajwa kama kati ya viungo mahiri zaidi kwenye kikosi
hicho cha Zesco ambacho kilifanya vizuri kwenye michezo ya Ligi ya
Mabingwa Afrika msimu huu na kuondolewa katika hatua ya nusu fainali.
Wakicheza
mchezo wa Ligi Kuu ya Zambia juzi kati ya Zesco na Mufulira Wanderers
ambao ulirushwa na Kituo cha SuperSport, mtangazaji wa mchezo huo
alisema kuwa kiungo huyo anakwenda Simba kwenye usajili huu.
“Huyu
anatakiwa na Simba ambayo ni kati ya timu kubwa za Tanzania, anaweza
kwenda kwenye timu hiyo,” alisema mtangazaji huyo wakati mchezo
ukiendelea.
Hata
hivyo, mchezaji huyo amekuwa akitajwa mara kwa mara kuwa anaweza
kujiunga na Yanga kwenye dirisha hili la usajili baada ya kocha wake,
George Lwandamina kujiunga na timu hiyo ya Jangwani.
Hata
hivyo, akizungumza na Championi Jumatano, mchezaji huyo amesema bado
hajazungumza na Simba wala Yanga, lakini yupo tayari kutua kwenye timu
yoyote.
“Sijazungumza
na timu yoyote ya Tanzania, lakini kama watakuja Simba au Yanga
nitajiunga nao, suala la msingi ni wenyewe kufuata utaratibu kwa kuwa
bado nina mkataba na Zesco,” alisema Chaila.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.