TANZANIA itaanza na Rwanda katika kuwania tiketi ya Fainali za Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) mwaka 2018 nchini Kenya.
Hiyo ni itakuwa katika Raundi ya pili ya mchujo wa michuano hiyo inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee na Taifa Stars itaanzia nyumbani Dar es Salaam kabla ya kuwafuata Amavubi Kigali.
Mechi nyingine kwa upande wa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati zitakuwa ni kati yaa Uganda na mshindi baina ya Somalia na Sudan Kusini zitakazomenyana katika Raundi ya Awali ya mchujo kati ya Aprili 20, 21 na 22 mwaka huu na kurudiana na kati ya Aprili 28, 29 na 30.
Djibouti itamenyana na Ethiopia, wakati Burundi itamenyana na Sudan na mechi za kwanza zinatarajiwa kufanyika kati ya Julai 14, 15 na 16 mwaka huu, wakati marudiano yatakuwa kati ya Julai 21, 22 na 23.
Ikifanikiwa kuitoa Rwanda, Tanzania itamenyana na mshindi kati ya Uganda na ama Sudan Kusini au Somalia katika Raundi ya Tatu ya mchujo mechi ya kwanza ikichezwa kati ya Agosti 11, 12 na 13 na marudiano kati ya Agosti 18, 19 na 20, mwaka huu.
Tanzania imewahi kushiriki mara moja tu fainali za CHAN, ambayo ilikuwa ni mwaka 2009 zikifanyika kwa mara ya kwanza kabia.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.