Walikuwa
ni Yanga walioanza kupata bao la kwanza kupitia Rafael Daud mnamo
dakika ya 57 baada ya kumalizia vema mpira wa adhabu na kuandika bao
hilo.
Mbeya
City walimka na kuanza kutafuta bao la kusawazisha, lakini walipatwa na
pigo kwa beki wake, Ramadhani Malima kutolewa nje kwa kadi nyekundu na
kubaki 10 Uwanjani.
Katika
dakika ya 93 zikiwa zimeongezwa 6 mpira kumalizika, Mbeya City walipata
bao la kusawazisha kupitia kwa Iddy Naddo aliyefunga kwa kichwa
kufuatia krosi safi iliyopigwa upande wa kulia mwa Uwanja.
Matokeo
hayo yanaifanya Yanga ijipatie alama moja pamoja na Mbeya City, ambapo
sasa imefikisha alama 48 kwenye msimamo huku watani zake wa jadi Simba
wakiwa na 59.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.