Baada ya kwenda sare ya bao 1-1 na Lipuli katika mchezo wa Ligi Kuu Bara, kikosi cha Simba kimerejea tena mjini Morogoro kuweka kambi maalum kwa ajili ya maandalizi dhidi ya Yanga.
Simba
imejificha Morogoro kujifua kabla ya kukabiliana na Yanga Aprili 29
2018, mchezo utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kikosi
hicho kimerejea mjini humo ikiwa ni siku kadhaa zilizopita kuweka kambi
ya muda mfupi wakati ikijiandaa na mechi dhidi ya Lipuli.
Wekundu
hao wa Msimbazi watakuwa wanaenda kuvaana na Yanga wakiwa vinara kwenye
ligi msimu huu, ambapo mpaka sasa wamefikisha jumla ya alama 59 huku
watani zao wakiwa na 47.
Wakati Simba ikiwasili Morogoro, Yanga wao wanacheza na Mbeya City leo kwenye Uwanja wa Sokoine, mjini Mbeya.
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.